Zoezi hili la usajili wa Wabunge wateule litafayika kwa siku tatu kuanzia tarehe 13-15 Novemba 2015.

Aidha mara ya baada ya zoezi la usajili kumalizika Wabunge wateule watapata briefing kuhusu shughuli za Bunge 

pamoja na kutembezwa katika maeneo mbalimbali ya Bunge tarehe 16 Novemba, 2015.

Mkutano rasmi wa kwanza wa Bunge la kumi na Moja ambao utaanza tarehe 17 Novemba kwa mujibu wa Kanuni za 

Kudumu za Bunge Toleo la April, 2013 kanuni ya 23 (1); Shughuli za Mkutano wa Kwanza wa Bunge jipya ni:

• Uchaguzi na Kiapo kwa Mhe. Spika
;
• Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wote
;
• Hoja ya Kuthibitisha Uteuzi wa Waziri Mkuu;

• Uchaguzi wa Naibu Spika

• Ufunguzi Rasmi wa Bunge Jipya utakaofanywa na Mhe. Rais


Chapisha Maoni

 
Top