Aliyekuwa spika wa bunge na mbunge mstaafu wa Urambo ndugu Samwel Sitta amesema kuwa hatothubutu kukubali kukatwa jina kizembe na chama chake cha mapinduzi kwenye kinyang'anyiro cha spika wa bunge kwa kutumika vigezo vya ubabaishaji.

Ndugu Sitta ameonya kuwa endapo kama chama chake kitatumia vigezo ili kuwabeba watu fulani kama ilivyofanyika mwaka 2010, atakimbilia mahakamani kufungua kesi ya kikatiba kupinga mchakato huo kuendelea.

Aidha Sitta amekiri kuwa katika kinyang'anyiro cha urais yeye alikatwa kwa kigezo cha umri mkubwa huku akionya jambo hilo lisitokee kwenye kinyang'anyiro cha uspika ndani ya chama chake. Sitta amechukua fomu ya kuwania kiti hicho leo kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba.