
Mechi ya kirafiki kati ya Ubelgiji na Uhispania ambayo ilikuwa imeratibiwa kuchezwa leo mjini Brussels Ubelgiji imeahirishwa kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea jijini Paris Ufaransa Ijumaa iliyopita.
Takriban watu 129 walipoteza maisha yao baada ya wavamizi wa kujitolea muhanga kujaribu kuingia katika uwanja wa Stade de France ambapo Ugerumani ilikuwa mgeni wa Ufaransa miongoni mwa maeneo mengi 5 jijini humo.
Maafisa wanaongoza shughuli za upelelezi tayari wamemtaja raia moja wa Ubelgiji kuwa ndiye aliyepanga njama hiyo ya uvamizi.
Serikali ya Ubelgiji tayari imeimarisha ulinzi ikihofia kutokea kwa shambulizi kama lile la Paris.

Shirikisho la kandanda la Ubelgiji limesema kuwa limechukua tahadhari hiyo kabla ya athari kufuatia mauaji ya zaidi ya watu 129.
Mechi hiyo ilikuwa imeratibiwa kuchezwa katika uwanja wa King Baudouin .
''kwa hakika hatuwezi kuhatarisha maisha ya wachezaji wetu na mashabiki,huu sio wakati wa kawaida''alisema afisa wa shirikisho hilo la Ubelgiji.
Vyombo vya usalama vimemtaja mzaliwa wa Ubelgiji Salah Abdeslam, mwenye umri wa miaka 26, kuwa mshukiwa mkuu
Chapisha Maoni