Image copyrightReuters
Image captionPolisi wamezingira eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis
Washukiwa wawili wamefariki baada ya maafisa wa usalama kushambulia Saint Denis kaskazini mwa Paris, wakisaka waliohusika mashambulio ya Ijumaa.
Ufyatulianaji mkali wa risasi umetokea mapema asubuhi kwenye mtaa huo. Operesheni hiyo inadaiwa kumlenga mwanamgambo wa Islamic State Abdelhamid Abaaoud ambaye amedaiwa kupanga mashambulio hayo yaliyoua watu 129.
Maafisa kadha wa polisi wamejeruhiwa kwenye operesheni hiyo, kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kimeripoti.

Chapisha Maoni

 
Top